Wengi husema kuwa Nandy amechukua nafasi ya Ruby. Hii ni kutokana na Ruby kuondoka THT ambako ndiko Nandy aliko sasa. Kingine mwaka jana Ruby alishiriki kwenye Coke Studio Afrika huku mwaka Nandy akienda pia. Pamoja na hayo, muimbaji huyo Na Yule, amempa ushauri muhimu muimbaji wa One Day.
“Nandy anatakiwa awe na moyo sana, yaani kila changamoto inayokuja kwake akabiliane nayo asikate tamaa, asonge mbele halafu amshirikishe sana Mungu kwa kila jambo,”
“Pia namshauri awashirikishe sana wazazi wake kwasababu yeye ana bahati ana wazazi wote wawili so awasikilize sana hao kuliko watu anaokutana nao njiani kwasababu sio wote ni wazuri. Kwahiyo namshauri awe tu karibu sana na wazazi wake zaidi pia aendelee kuwa real asije kutamani kuishi maisha ya mtu mwengine,” ameongeza Ruby
Ruby pia amewashukuru mashabiki zake ambao bado wanaendelea kumsapoti na amewaahidi baada ya Ramadhani atawaletea kazi mpya.
Source: Dizzimonline