Rama Dee Asema Sina beef Na Adam Juma

Msanii wa muziki, Rama Dee amedai kauli yake “Hanscana ni muongozaji mkali wa video kuliko Adam Juma” siyo kama alimkosea heshima muongozajii huyo mkongwe wa video za muziki.

Muimbaji huyo amedai alitaka kumwambia ukweli muongozaji huyo ili kama anaweza kubadilka abadilike.

“Sikujenga beef na Adam Juma, nilisema kitu ambacho nakiona,” Rama Dee alimjibu mmoja  kati ya mashabiki wake ndani ya Kikaangoni EATV.  “Kwanini nimwambie kwa siri, hakuna cha siri, mtu akizungua unamwambia moja kwa moja,”

Aliongeza, “Mimi sina beef na mtu, mimi nafikiri mtu akiambiwa ukweli anatakiwa kutulia siyo na wewe unanza kutafuta namna ya kujitetea,”

Muimbaji huyo amedai hataki kuzungumzia zaidi mahusiano yake na Adam Juma kwa kuwa tayari ameshamalizana naye.

Hata hivyo kauli hiyo ya ‘Hanscana ni mkali kuliko Adam Juma’, ilipingwa na wadau mbalimbali katika mitandao ya kijamii wakidai muimbaji huyo amemkosea heshima Adam Juma.

Source: Udaku