Orodha ya wafanyakazi wenye vyeti feki Hospitali ya Muhimbili

Ishu ambayo ilichukua headlines hivi karibuni ni kuhusu vyeti feki baada ya ripoti kukabidhiwa kwa President Magufuli ambapo alitoa agizo kuwa wote waliotajwa kwenye orodha kuondoka kazini mara moja.

May 8 2017 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wametoa Tangazo lililoambatanishwa na orodha ya wafanyakazi waliobainika kuwa wameghushi vyeti vyao vya elimu ya Sekondari hivyo wametakiwa kujiondoa wenyewe kazini ifikapo May 2017.

Taarifa hito imeeleza kuwa endapo kuna wafanyakazi hawajaridhika na uamuzi huo, imeelekezwa wakate rufaa kwa katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kabla ya May 15 2017 na barua zipitie kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ya maoni yake.

Aidha angalizo limetolewa kuwa Wakuu wa Idara/Majengo wanatakiwa kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanaohusika hawaendelei kutoa huduma. Nimekuwekea hapa orodha ya waliobainika kuwa na vyeti feki Muhimbili.

Source: Millard ayo