Rapper Mystikal akamatwa na polisi.

Rapper Mystikal amekamatwa na kushtakiwa kwa kosa la ubakaji huko Shreveport, LA nchini Marekani. Kwa mujibu wa TMZ, mchanaji huyo wa New Orleans amejisalimisha mwenyewe polisi baada ya kupewa waranti wiki iliyopita.

Rapper huyo anadaiwa kumshambulia kimapenzi mwanamke kwenye kasino mwaka 2016. Ripoti zimedai kuwa wapelelezi walibaini DNA kushabihiana na ya rapper huyo mwenye miaka 46 na ambaye jina lake halisi ni Michael Tyler.

Mwanaume mwingine, Averweone Holman, pia amekamatwa kwa kuhusika na tukio hilo. Dhamana yao imetajwa kuwa ni dola milioni 2 kila mmoja. Rapper huyo anakana mashtaka.

Hii si mara ya kwanza rapper huyo anakamatwa kwa kosa la aina hiyo. Aliwahi kufungwa miaka 6 kwa kosa la ubakaji na kutoka mwaka 2010.

Source: Dizzim Online.