Vita Kubwa Kati Ya Mobeto Na Zari.

HALI si shwari kati ya mwanamitindo matata wa Bongo, hamisa hassan Mobeto na mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki ambaye ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Zarinah hassan ‘Zari The Boss Lady’, kisa kikielezwa kuwa ni mtoto.

Wakati mtoto huyo wa Mobeto aliyepewa jina la baba mzazi wa msanii huyo akitimiza siku 14 leo Jumatatu, uzao huo umesababisha Mobeto kuibuka na kicheko kwa kuungwa mkono na Wabongo huku Zari akidaiwa kuambulia kilio kutokana na kushambuliwa mitandaoni.

Mara tu baada ya Mobeto kujifungua mtoto huyo Agosti 8, mwaka huu, Zari alitokwa na povu ambalo siyo la nchi hii huku akipiga mkwara kuwa asihusishwe na mtoto huyo wa ‘bitch’ (malaya), kauli ambayo aliitoa kupitia ukurasa wake unaotambuliwa kwenye Mtandao wa Instagram. Kilichofuatia ni majibizano ya mashabiki wa Mobeto na wale wa Zari ambapo kila upande ulikuwa ukivutia upande wake, lakini pande zote zilichukizwa na neno ‘bitch’ ambalo ni tusi lililotumiwa na Zari kwenda kwa Mobeto ikielezwa kuwa lilitokana na hasira.

JINA LA BABA MkWE
Wakati mambo yakiwa hayajakaa sawa huku mtoto huyo wa pili wa Mobeto akiibua tafrani ya aina yake mitandaoni, mwanamitindo huyo aliibua lingine baada ya kumpa mtoto huyo jina lililodaiwa kuwa ni la baba mkwe wa Zari. Inasemekana kwamba, jambo hilo ndilo linalodaiwa kuthibitisha kuwa Mobeto amezaa na mwanaume huyo hivyo kuibua shangwe kwa Wabongo na kumuongezea machozi Zari.

Ilielezwa kuwa, jina hilo, ndilo lililomaliza maswali mengi ya mashabiki ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo. Awali, Mobeto alifungua akaunti kwenye Mtandao wa Instagram kwa jina ‘Tanzania Baby’, lakini baadaye wiki iliyopita alibadilisha jina hilo ambapo hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, akaunti hiyo ilikuwa ikikaribia kuwa na wafuasi (followers) laki moja.

MAMA MZAZI NA DADA MTU
Tukio lingine lililoibua gumzo juu ya mtoto huyo ni kufuatia kitendo cha mama mzazi wa jamaa huyo na dada yake kuonekana kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye hospitali ambayo Mobeto alijifungulia, ikidaiwa kuwa walifuata damu yao ambayo ni nzito kuliko maji.

Hata hivyo, jambo lingine lililozungumzwa zaidi ni kitendo cha jamaa huyo kumkana Mobeto ikidaiwa kuwa alilenga kumpooza Zari ambaye inasemekana jambo hilo lilimtibua mno na kumtaka jamaa huyo aliyezaa naye watoto wawili kukanusha kuzaa na Mobeto.
mobeto na zari
Mobeto.

MOBETO APIGWA STOP
Katika mazingira hayo, mtu wa ndani ya familia ya mwanaume huyo alilitonya Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa Mobeto amepigwa ‘stop’ (marufuku) kufanya mahojiano na waandishi wa habari.

Hata hivyo, Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa Mobeto, maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar ambapo mara baada ya kujitambulisha lilifungiwa mlango wa geti kwa madai kwamba, waandishi hawahitajiki.

WAZAZI FULL RAHA
Kwa upande wao, wazazi wa mwanaume huyo anayedaiwa kuzaa na Mobeto, wamepokea baraka hiyo kwa mikono miwili huku babu mtu akifurahia zaidi mtoto huyo kupewa jina lake. 40 YA kiShiNDO Hata hivyo, taarifa zilizofika muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilieleza kwamba, familia ya Mobeto yaani mama yake ipo kwenye mipango kabambe ya kuandaa 40 ya mtoto huyo kwani itakuwa haijawahi kutokea Bongo. Tusubiri.

                                                                                           Source: Udaku
Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!