OMOG afuku­zwe’, ‘Omog abaki’, ‘Omog hatufai’, ‘Omog ni tatizo’, ‘timu haziche­zi vizuri tatizo ni Omog’.

OMOG afuku­zwe’, ‘Omog abaki’, ‘Omog hatufai’, ‘Omog ni tatizo’, ‘timu haziche­zi vizuri tatizo ni Omog’.

Hizo ni baadhi ya kauli ambazo zimekuwa zikita­wala kwenye vyombo vya habari, mitandaoni, kwenye vijiwe na kwingine kote am­bapo kuna mazungumzo kuhusu Klabu ya Simba.

 

Simba ipo katika nafasi ya nne ikiwa imezidiwa pointi mbili na Mtibwa Sugar am­bayo inashika usukani katika Ligi Kuu Bara, pointi za Simba ni sawa na zile za wapinza­ni wao wa jadi, Yanga, wote wakiwa wameshinda michezo miwili na kupata sare mbili.

 

Ubingwa unawaniwa na timu zote lakini Simba kunaweza kuwa na presha kubwa zaidi ya timu nyingine zote kutokana na mazingira halisi ya timu hiyo hasa ni kutokana na kutumia ki­wango kikubwa cha fedha ka­tika usajili, pili ni kiu ya kuu­taka ubingwa wa ligi hiyo baada ya Yanga kutawala kwa miaka kadhaa.

 

Omog ame­wahi kuipa ub­ingwa Azam FC, pia ndiye aliyei­wezesha Simba kupata nafasi ya kurejea ka­tika michuano ya kimataifa, kwa wasifu wake katika soka la Afrika sina shaka na uwezo wake wa kufundisha hasa ukizingatia aina ya mazin­gira ambayo anafundishia.

story@moodyhamza