Nyota wa filamu Sylvester Stallone amekana ripoti kwamba yeye na mlinzi wake walimnyanyasa kingono shabiki wake

Nyota wa filamu Sylvester Stallone amekana ripoti kwamba yeye na mlinzi wake walimnyanyasa kingono shabiki wake wa miaka 16 mjini Las Vegas mapema miaka ya themanini.

Gazeti la mtandao la The Mail limechapisha kile linasema ni ripoti ya polisi kutoka 1986 ambayo ilielezea madai hayo.

Mwanamke huyo hakuwasilisha mashtaka dhidi ya Stallone kwa sababu alinyanyaswa na kuaibishwa mbali na kuwa na hofu.

Hakuna hatua iliochukuliwa.

Msemaji wa nyota huyo wa filamu ya Rocky alisema kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya uwongo.

Michelle Bega aliyaelezea madai hayo kuwa ya uwongo, akiongezea : hakuna mtu aliyekuwa akijua kuhusu habari hiyo hadi ilipochapishwa leo, akiwemo bwana Stallone.

”Bwana Stallone hakuwasiliana na mtu yeyote ama mamlaka  yeyote  kuhusu swala hilo”.

@moodyhamza