Nay wa Mitego Amteka AY.

 

Msanii Nay wa Mitego ‘amemteka’ msanii mkongwe wa bongo fleva AY ‘Mzee wa Comercial’ na kuibuka naye katika studio yake ya Free Nation jambo linalozua maswali kuwa huenda kuna kazi ya pamoja ambayo wawili hao wanafanya.

Nay amewaweka njia panda mashabiki na wapenzi wa muziki wake kwa kitendo cha kuweka picha katika mtandao ambayo inamuonesha msanii huyo akiwa ndani ya studio za Freenation pamoja na AY.
‘With ma Big Bro AY Guess Wat’…#FreeNationRecords #MudaWetu. Ameandika Nay wa Mitego katika ukurasa wake.

Imekuwa ndiyo ‘style’ ya mjini siku hizi kwa baadhi ya wasanii wakitaka kufanya ‘remix’ na msanii mkubwa lazima utaona anaanza kuwa ‘attention’ mashabiki zake kwa kuweka picha mtandaoni ikiwa inawaonesha wakiwa studio hata wengine wakiwa karibu katika masuala ya kijamii ili mradi tu wananchi waongee kwa upande wao.

Source: Udaku