Nandy Vanessa wanafanya vizuri lakini siwahofii.

Baada ya kufanya TOUR ya kimuziki katika miji ya Mombasa na Nairobi, Kenya Mwimbaji staa Lulu Diva kutoka Bongoflevani amekaa na Ayo TV na milladrayo.com na kuelezea mapokezi makubwa ambayo hakuyategemea.

Mbali na kuelezea tour yake hiyo Lulu Diva amezungumzia pia uwezo wa baadhi ya waimbaji wa kike wa Bongofleva akiwataja Vanessa Mdee, Nandy na Maua Sama akisema wanafanya vizuri na wana uwezo lakini hawahofii.

Kati ya Nandy na Vanessa hakuna ninayemuhofia kukaa nafasi yangu. Sijui Watanzania wenyewe ndio wanaofahamu ukweli kabisa. Nandy anafanya vizuri kwa nafasi yake na Vanessa anafanya vizuri kwa nafasi yake, hata Lulu Diva anafanya vizuri kwa nafasi yake. Maua atabaki kuwa Maua hata kama atajitokeza mtu na kujifanya kama Maua Sama.” – Lulu Diva.

Source: Millard ayo