Masogange Atoa Povu Kwa Wenzake.


Video Queen mkongwe, Agnes Masogange ametamka kwamba sasa ameamua kuachana rasmi na kuuza sura kwenye video kwa vile baby wake hapendi huku pia akitaka watu kuacha kufikiria kwamba anafanya biashara kujiuza.

“Watu bana!, mimi sina dhiki ya kufikia kuuza mwili wangu eti nipate pesa na kuhusu zile picha kipindi kile nilizopiga hazikuwa za utupu sema basi tu watanzania tunapenda kuzusha sana. Na mtu kuenda Sauzi ndio ameenda kujiuza?,” Masogange aliliambia Gazeti la Mwanaspoti.

Aliongeza, “Mimi nilikuwa na biashara zangu nafanya na wanaosema hivyo hawanisaidii chochote,hakuna mtanzania anayeninunulia nguo,hayupo anayenipa pesa waongee tu. Unajua sisi wadada tuna tabia ya kuoneana wivu akiona unafanya vizuri anaanza kukusemea vitu vya ajabu pembeni,”anasema msanii huyo na kuongeza kwamba amepima ukimwi yuko safi,”

Katika hatua nyingine mrembo huyo alikana kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kama baadhi ya watu wanavyodhani.

 

Source: Udaku.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!