Msanii Ommy Dimpoz Amepoteza.


MUBENGA aliyekuwa meneja wa msanii, Ommy Dimpoz, ameibuka na kusema kuwa tangu aache kumsimamia msanii huyo, amepoteza dira kimuziki, ndiyo maana hatoi nyimbo kwa wakati.

“Tukizungumza kwa namna ambavyo mimi nimefanya kazi na Ommy, vitu vingi vinavyomtokea sasahivi sielewi hata mimi nashangaa, kwa sababu ukiangalia hata kwenye gemu yetu hafanyi vizuri tena, sijui anakosea wapi, hata kazi zake hazina ubora na hazitoki kwa wakati.
“Nakumbuka wakati tunafanya kazi kuanzia Nai Nai, Baadaye, Ndagushima, Me and You, Tupogo, Wanjera ni nyimbo ambazo zilikuwa zinatoka kwa wakati, na mapokezi yake yalikuwa ni makubwa sana.

MUBENGA aliyekuwa meneja wa msanii, Ommy Dimpoz
Dimpoz Alivyosaini Katika Label Rockstar
“Sijui labda yeye mwenyewe anajiona wapi, lakini mimi simuoni pale ambapo nilikuwa nimemfikisha,” amesema Mubenga.

Baada ya kutemana na Mubenga, Ommy Dimpoz kwa sasa yupo chini ya menejimenti ya Rockstar, ambayo ndiyo inayomsimamia Ali Kiba.

Source: Udaku.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!