Jux amewajia juu watu wanaojadili sana kuhusu wanaume wanaopiga picha na mpenzi wake Vanessa Mdee.
Hitmaker huyo wa ‘Umenikamata’, amesema yeye wala haumizwi na picha hizo kwa kuwa anafahamu kuwa mrembo wake huyo yupo kazini kwani hata yeye anafanya kama hivyo na inaonekana ni kawaida?
“Si kweli mimi nilimind, sababu kama kupiga picha za namna hizo Vanessa anapiga na watu wengi sana picha za namna ile. Naomba nirudi nyuma kusema hili tena wasichana kwenye tasnia yetu sisi wavulana ndiyo tunatakiwa kuwasupport sana kwa sababu wapo wachache,” amesema Jux.
Muimbaji huyo ameongeza, “Mimi hata nikipiga picha na wanawake 10 hapa, watu watajua tu Jux anafanya video ila Vanessa akipiga picha hizo watu watasema huyu mwanamke mhuni.”
Source: Udaku