Msanii Kajala Ashutumiwa Tena.


Kufuatia uwepo wa tuhuma kwamba anaongoza kwa kukwapua mabwana wa watu, muigizaji kiwango, Kajala Masanja ameibuka na kukanusha vikali madai hayo na kusema anayachukia.

Kajala alisema watu wamekuwa wakimwita nyakunyaku na yeye halipendi hilo jina hata kidogo ni bora skendo zote azipitie lakini sio hiyo ya kuiba wanaume za watu.
“Hakuna kitu ninachokichukia kama mtu kuniona mimi ni wa kuchukua mabwana za watu na kunifananisha na nyakunyaku, nakereka mno,” alisema Kajala.

Katika historia yake ya maisha, Kajala amekuwa akihusishwa kukwapua bwana wa Wema Sepetu, maarufu kama CK pamoja na msanii wa Bongo Fleva.

Source: Udaku.

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors