Mr Blue Abadilisha Staili Ya Kurap.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Ama G. Chotara anayefanya vizuri na ujio wake wa ngoma ‘Mwambie’ aliyomshirikisha fundi wa uandishi na michano Mr. Blue ametoa sababu za kumbadilika na utofauti wa michano aliyofanyaka katika ubeti wa Mr. Blue  Ama G amesema kuwa Byser alicholenga ni kufanya kikubwa cha tofauti na alichozoeleweka kufanya katika kolabo zake za siku zote ambapo pia fanya kwa lengo la kuongeza nguvu kubwa nay a tofauti kwa msanii ambaye aliamini kuwa uelekeo wake ni mzuri.

“Mr. Blue kabadilika kwenye hii ngoma kutokana na utofauti wa beat ya huu wimbo wangu mpya, na siku ya kwanza anakuja kurecord aliniuliza kama aimbe ama arap na mwisho wa siku baada ya kuamua kuimba alifanya kitu kikubwa  namshukuru sana kwa hiki alichokifanya kwasababu hata pale studio wengi walionekana kupenda sana hicho cha tofauti alichokifanya mara tu alipomaliza kurecord” Alisema Ama G.

Hata hivyo inaweza kuaminika kuwa kila msanii ambaye anapata nafasi ya kushirikiana na Mr. Blue upata jeki kubwa ya kusikilizwa na wapenzi wa muziki mzuri kwa maana ya uwezo anaouonesha katika kila kolabo analofanya.

Source: Dizzim Online