Moja kati ya stori ambazo zilitrend kwa muda mrefu katika mitandao ya kijamii ni pamoja na kundi la muziki wa Bongo Fleva Yamoto Band lenye makazi yake Temeke kujengewa nyumba za kuishi na kiongozi wao ingawa hawajakabidhiwa.
Leo April 25 2017 kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM staa wa TMK Wanaume Family Mh. Temba ambaye pia ni kiongozi wa Yamoto Band amezungumzia kuhusu ucheleweshwaji wa kukabidhiwa nyumba zao ingawa wasanii hao wameshakuwa watu wazima ambao wanaweza kujitegemea.
Mh. Temba alikwenda mbali zaidi akisema kuwa wanamuziki hao wameshakuwa watu wazima hivyo hata fedha zao wanatakiwa wapewe wenyewe ili wajue kwamba sasa wamekuwa wakubwa na kama watazitumia vibaya, basi yatakuwa juu yao lakini wanatakiwa kumalizia nyumba zao kwa sababu ni vitu vidogo tu ambavyo vimebakia kama maji na umeme.
“Tumeongea na mangement kuwa, hawa Yamoto wanatakiwa wajitegmee wenyewe. Wameshakuwa wakubwa. Kama mtu utampa hela zake akaenda kufanya starehe, atajua mwenyewe. Nyumba zimeshakamilika ila wanatakiwa wamalizie wenyewe vitu vidogo ili wajue uchungu wa kuhangaika.
“Nyumba, wanaweza kuishi, kwa sababu vitu ambavyo hakuna ni Tiles, umeme na maji kwa sababu maji kule hayajafika. Sikutakiwa kukuelezea ila nimekuelezea tu kwa kuwa maswali yamekuwa mengi.
“Wanatakiwa wahamie sasa hivi maana hata sisi tulihamia kwenye nyumba zetu wakati hazina maji wala umeme. Kwa hiyo wahamie wajue wameshakuwa baba wa familia. Kuwa baba sio mchezo.” – Mh Temba.
Source: Millard ayo