Siku chache zilizopita mwanadada Linah Sanga alichafua hali ya hewa katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kuawa anapost picha/video za Idris Sultan huku akiambatanisha na caption zenye utata ukizingatia Idris alikuwa ni mpenzi wa mwanadada Wema Sepetu.
Moja kati ya caption za Linah ambazo zilizua gumzo sana mtandaoni ni ile aliyoandika “Mungu alituumba sote Why na sisi tusipendane???” huku akiwa ametupia na picha ya Idris kitu ambacho kiliipelekea post hiyo kupata comments zaidi ya elfu moja (1,000).
Mengi yalizungumziwa baada ya sakata hilo ikiwemo na kuwa mwanadada Linah kwa sasa anatoka kimapenzi na Idris. Kama umekuwa ukifuatilia post za Linah utagundua kuwa mwanadada huyo alikuwa akipokea kichambo sio cha kitoto kutoka kwa mashabiki wa Wema Sepetu ukizingatia mwanadada Wema ni mmoja kati ya wanawake wenye ushawishi mkubwa sana barani Afrika.
Ikiwa bado hilo la Idris linaelea elea Linah ameamua kuja na jingine tena la kupost picha akiwa na mwanaume ambaye hamuonyeshi sura yake kamili. Ni mengi yanaongelewa katika mtandao huo na moja kati ya post hizo ni hii hapa.
Siku hizi imekuwa kama imezoeleka hivi kwa baadhi ya wasanii pindi watakapo kufanya yao huwa wanakuja kama na kiki hivi ili kujitengenezea mazingira flani kwa muda huo waweze kuzungumziwa kwa malengo ya mipango yao iweze kupenya. Sina uhakika sana kuwa kwa mwanadada Linah na hii pia ni kiki au la.
Story By:@Joplus_
Source: Perfect255.com