Kuna Wasanii Wakitoa Ngoma Huwa Situlii

Staa wa ngoma ya “Ukivaaje Unapendeza” Dogo Janja amewataja wasanii ambao akisikia wanatoa ngoma huwa akili yake haitulii na anashindwa kufanya mambo yake.

Dogo Janja ambaye amekulia kimuziki kwenye mikono ya Madee, ameiambia Dizzim Online kuwa yeye haogopi kutoa ngoma siku moja hata na Jay Z lakini kuna wasanii ambao akisikia wanataka kutoa ngoma husita kufanya chochote.

“Yani mimi kuna wasanii wakisema wanataka kutoa nyimbo basi daah nakuwa situlii kabisa kutaka kujua hiyo ngoma itakuwaje ni Joh Makini, Mwana FA, ni watu ambao wakitaka kutoa ngoma huwa nakuwa na hamu sana ya kutaka kujua wameimba nini. Kwasababu ni vinyonga kwenye game yao yaani kila siku wao wanabadilika, so hao ni watu ambao nawatolea macho sana,” amesema rapper huyo.

Source: Dizzim online