Kilichoendelea leo mahakamani kwenye kesi ya Agnes Masogange

Video Queen Agness Gerald maarufu kama ‘Masogange’ ambaye ametokea kwenye video kadhaa za muziki wa Bongofleva,  alikwenda Mahakamani Kisutu Dar es salaam kufuatia kuitwa Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa wakili wake aitwae Nictogen Itege  ameiambia millardayo.com kuwa kesi imeahirishwa mpaka tarehe 20 mwezi April kwasababu upande wa Serikali bado haujakamilisha Upelelezi juu ya kesi ya Video Queen huyo.

‘Leo kesi ilikuwa mara yake ya mwisho kutajwa lakini imepangiwa tarehe nyingine ambayo imepangiwa tarehe 20 mwezi April kama alivyosema mheshimiwa kuwa Serikali bado hawajakamilisha upelelezi  kwa hiyo hayo ndio naweza kukuambia kwa sasa’

Source: Millard ayo