JAZA ujazwe! Habari ya mjini kwa sasa inamhusu sexy lady wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ kujazwa kibendi na staa mkubwa wa muziki huo, licha ya kwamba mwanadada huyo amekuwa akifanya siri.
Chanzo makini kililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, Ruby ana ujauzito ambao umekuwa ukimfanya ajifichefiche huku akimficha aliyemjaza kibendi hicho kwa madai kuwa, jamaa aliyempachika kibendi amezaa na wanawake tofauti.
Kama ilivyo desturi yake, Ijumaa Wikienda lilimnyatia Ruby ambaye alikiri kuwa mjamzito, lakini akatia ngumu kumtaja baba kijacho na umri wa mimba yake kwani wakati muafaka haujafika.
“Mimba bado ni changa, siwezi kusema ina miezi mingapi. Kuhusu nimepewa na mwanamuziki mkubwa, siyo kweli ila ipo siku wakati ukifika nitasema ni ya nani,” alisema Ruby
Source: Udaku