Ili Uwe na Sifa ya Kujiunga na WCB Lazima Uwe na Uwezo Huu

Rais wa lebo ya WCB Diamond Platnumz amefunguka na kusema ni vigumu kwa msanii kujiunga na lebo yake hiyo kama hajui kuandika nyimbo.

Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa wimbo unapoandikwa ndani ya lebo hiyo mara zote unakaguliwa na watu wote ili kubaini kama kuna makosa na kuelekezana.

“Kwanza Rich Mavoko ndiye mgumu kwenye kupitisha nyimbo, ikitoka hapo Ravvanny aipitishe, Queen Darleen aipitishe, ikitoka hapo niipitishe mimi, iende kwa Mkubwa Fella na Babu Tale waipitishe na Sallam aipitishe, ukitoka hapo wewe ni mwanaume haswa,” amesema Rich Mavoko na kuongeza.

“Kwa hiyo wengi wanakuwa na uwezo mkubwa. Labda unaweza ukaja ukasikia kitu kidogo, ukasema ukiweka hapa kitu flani itakuwa poa zaidi, yaani ukiandika unaandika haswa,” ameeleza Diamond.

Source: Udaku