Walichoandika mastaa Bongo miaka minne tangu Mangwea afariki


May 28 ni kumbukumbu ya kifo cha Mfalme wa Freestyle kutoka Bongo Albert Mangwea ambaye May 28, 2017 ametimiza miaka minne tangu afariki. Watu mbalimbali wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuandikia sala zao pamoja na namna walivyomfahamu Mangwea.

Taarifa za kifo cha Albert Mangwea zilisambaa mchana wa May 28, 2013 ambapo kulingana na ukubwa wa jina lake Tanzania hakuna aliyekuwa tayari kuamini kama ni kweli amefariki lakini baadaye ilithibitika kweli Mangwea amefariki dunia.

Producer P Funk Majani alipost Picha 12 mfululizo za kukumbuka kifo cha Ngwea na kuandika: “You will never be forgotten brother 🙏🏽”  (Hautasahaulika milele kaka 🙏🏽)

Source: Millard ayo