Mikoba ama mapochi imetokea kua kiungo muhimu sana kwenye mitindo kwa wanawake zaidi lakini pia kwa baadhi ya wanaume.
Tukisema hand bag ya kisasa ni ile inayokwenda na msimu au trend. Ipo mikoba au hand bag nyingi na za aina tofauti, ila jua vitu muhimu vya kuwa navyo wakati wa kuchagua mkoba bora, wa aina gani na wakati gani.
Kama mwanamke wa kisasa, unatakiwa uwe na mikoba mizuri na yenye kuvutia. Wingi wa mikoba katika chumba chako haimaanishi ubora. Hakikisha katika list ya mikoba ulionayo, haukosi rangi muhimu kama vile nyeusi,Brown na Nyeupe.
Kabla ya kununua mikoba hakikisha unajua bei ya mikoba hiyo na bei yako lazima ifafanie uimara, kwani kwa mikoba, uimara ndio kila kitu.
Source: Udaku