Dogo Janja aingilia kati mapenzi ya Harmonize na Wolper

Msanii kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amesema licha ya kuwaimba Harmonize na Wolper katika wimbo wake wa Kidebe, hajawahi ‘kuvutiwa’ na mahusiano yao.

Dogo Janja amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa msanii akishakuwa kwenye mahusiano na mtu maarufu ni lazima akubali mapenzi yake kufuatiliwa na watu wengi.

“Ukishakuwa na mpenzi staa hiyo ni flamu tayari, maisha yenu ni filamu watu wanafuatilia. Kingine mapenzi yao yalivyokuwa yananza watu walikuwa wanachukulia kama Drama lakini mwisho wa siku unakuja kuona kama wapo serious, kwa hiyo ni vitu kama hivyo.

“Mimi kama mimi siko interested nao sana, ni verse tu zile, siko interest nao kwa vile na mimi nina mapenzi yangu , kila mtu ana mitikasi yake” amesema Dogo Janja.

Siku za hivi karibuni kuliibuka uvumi kuwa wawili hao wameachana lakini baadae Harmonize alikuja kuthibitisha ukweli kuwa hawapo tena pamoja.

                                                        Source: Udaku