Alikiba aelezea kwanini M.I hajaonekana kwenye video ya Aje, asema walimkatia tiketi mbili za ndege lakini hakutokea


Alikiba ameelezea sababu za kwanini rapper wa Nigeria, M.I hakutokea kwenye video yake ya Aje Remix.

Alikiba amesema mara ya kwanza alilazimikia kubadilisha na kuimba kifaransa sehemu ambayo alikuwa ameimba M.I baada ya ratiba yake kuwa ndefu, lakini hadi kwenye remix hakufanikiwa hivyo akaamua kushoot tu mwenyewe.

“Hatukutaka kuingilia ratiba zake kwahiyo sisi tuliweza kufanya ile ya Kifaransa tukamaliza video. Lakini hii ya sasa hivi vile vile tulijitahidi kwa nguvu zetu zote kuhakikisha M.I atakuwepo lakini kuna sababu ambazo sisi wenyewe, management yangu ziko nje ya uwezo wetu,” alisema Kiba.

“Sababu tuliweza kukata tiketi mara mbili, namaanisha siku mbili tofauti, licha ya kutumiwa tiketi kwa mara ya kwanza bahati mbaya akakosa ndege na siku ya pili tena ikakosekana ndege. Kwahiyo kibinadamu tu haipendezi, sio kwamba kuonesha tuna hela ama nini kwamba tumtumie tena tiketi ya tatu, tukaona haina shida, we can do this,” aliongeza.

SOURCE BY: TEENTZ