CHRIS AGOMA KUIMBA WIMBO WA TAIFA.

Wimbo wa taifa ni moja ya nyimbo ambazo zinahitaji kupewa heshima kubwa, Chris brown kwake nyimbo ya Taifa ni ujinga tu kwake.

Tokeo la picha la chris brown refuse to stand up in anthem song

Chris Brown ni moja ya wasanii ambao majina yao tayari yashakuwa vinywani mwa watu kutokana na kila kukicha kuandamwa na matukio ya kushangaza, hivi karibuni Chris Brown ameshangaza mashabiki wake baada ya kugomea kusimama pale wimbo wa Taifa ulipokuwa unapigwa katika mchezo wa 106’s All Start Celebrity Game wakati wa kuadhimisha tukio la September 9/11.

Kupitia video iliyonaswa na mtandao wa Tmz umeonyesha msanii Chris brown akiwa amekaa chini wakati wimbo wa taifa ukiwa unapigwa kwa ajili ya kuwakumbuka watu waliofariki miaka 15 iliyopita katika shambulizi la Kigaidi

Story by:@Joplus_

Source:Perfect255.com