B. Dozen ampa shavu Dj Fetty.

Mtangazaji wa Clouds FM, Hamis Mandi aka B12, amesema co-host wake wa zamani wa kipindi cha XXL, Dj Fetty, ni mtangazaji smart zaidi wa kike wa vipindi vya burudani Tanzania.

Mtangazaji huyo anayejulikana pia kama B-Dozen, amesema kuondoka kwa Fetty katika redio hiyo, kulimfanya adhani kuwa show ya XXL isingekuja kuwa na mvuto tena.

“Fetty is one of the smartest female presenters ambao nimewahi kuwajua wanaofanya entertainment,” Dozen aliiambia Podcast ya Nje ya Box ya Pascal Kadushu inayoruka kupitia Afripods.

“Sidhani kama kuna mtu mpaka sasa hivi ameifikia level ya Fetty,” amesisitiza.

“Mwanzoni alipoondoka Fetty nilifikiri kwamba hatutaweza kuwa kama ambavyo tumekuja sasa hivi. Imetuchukua muda mrefu kama umetugundua, hatukuwa na chemistry hiyo. Chemistry yangu ya Adam na Fetty ilikuja automatic sababu tuliajiriwa almost kipindi kimoja halafu tuko the same age, wote tunapenda vitu vinafanana ile kuhang pamoja ikatengeneza chemistry ambayo kiukweli hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuivunja, ilikuwa ni chemistry ya kipekee.”

Source: Dizzim online.