Haijawahi kutokea Tanzania kwa miaka 10
Msemaji wa TFF Alfred Lucas asema uwanja wa Taifa Dar umejaa, hivyo walioko nje warudi kwao. Ataka walioko nyumbani wasiende Taifa. Hatua hiyo imekuja Kufuatia mashabiki kufurika uwanjani na wengine kuzuiwa kuingia kutokana na uwanja kujaa, TFF imewataka mashabiki walioko ndani kuwapigia simu ndugu na rafiki zao wa nyumbani kutokwenda uwanjani kwani kumejaa na hawataruhusiwa kuingia.Haijawahi kutokea Tanzania kwa miaka 10 iliyopita kwa mashabiki kuingia uwanjani kuanzia saa 3:00 asubuhi kwa lengo la kushuhudia mechi ya Yanga dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Licha ya TFF kueleza milango ya uwanja huo kufunguliwa saa tano asubuhi, lakini walilazimika kuifungua saa tatu asubuhi kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo na kuingia moja kwa moja uwanjani. Ofisa huyo wa habari wa TFF , alisema walilazimika kufungua milango ya uwanjani mapema tofauti na walivyoeleza awali kutokana na mashabiki kufurika uwanjani kuanzia saa tatu asubuhi.
story@moodyhamza