Kundi La P.square Lina Mgogoro Mkubwa Sana.

Kundi hilo lililofanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano linadaiwa kuvunjika rasmi baada ya wawili hao kuingia katika mgogoro mpya. Imeripotiwa kuwa Peter ameshatuma mwanasheria wake Festus Keyamo kwa ajili ya kuweka makubaliano ya kundi na tayari huku akikurundika madai yake kwa pacha wake Paul na meneja wao ambaye ni kaka yake Jude.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa Peter amekuwa akimshawishi kaka yake(Paul) wafanye kazi lakini kaka yake huyo ameonyesha kutokuwa na ushirikiano pia imeongeza kuwa, Paul alikatisha safari za muziki wa kundi Amerika Kaskazini bila ya kumshirikisha.

Pia ripoti ikaongeza kuwa Paul amekuwa akiwatumia familia yake (Mke na watoto) katika mitandao ya kijamii kwa madai kuwa wekuwa wakipokea ujumbe wenye vitisho kutoka kwa Peter. Ripoti pia ikaongeza kuwa meneja kundi hilo amabye ni kaka yao Jude Okoye aliwahi kumtishia kumpiga bastola Lola.

Kutokana na ripoti iliyotolewa na Peter kupitia kwa mwanasheria wake, Peter amesema imetosha na hawezi kuendelea kufanya kazi sehemu kama hiyo hivyo ameamua kufanya kazi mwenyewe kama Mr P.

Source: Udaku.