, “Wanadamu wote hukosea na kutenda hambi,

Kulingana na mafunzo ya dini ya Kiislamu, dhambi ni kitendo kinachofanywa kinyume na sheria na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Mtume wetu Muhammad (S.A.W) anaelezea dhambi kuwa kama , “Kitendo ambacho hakuna mwanadamu yeyote anayependa kukifanya wala kukiskia.”[1] Toba nayo ni hali ya mwanadamu kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya kuomba msamaha. Wanadamu hutenda dhambi kwa makusudio na wakati mwengine hutenda pasi na makusudio. Hivyo basi wao hujirudi na kuomba msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa dini Kiislamu, wanadamu huaminika kutozaliwa na dhambi ila katika maisha yao wao hutenda dhambi. Wanadamu pia wamepewa mwongozo na mafunzo yanayoweza kuwaepushia vitendo vya dhambi au kujikinga na ukiukaji wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Hakuna mwanadamu aliyekamilika na kuishi pasi na kukosea. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu huweza kumsamehe yule anayejirudi na kuomba msamaha.  Mtume wetu Muhammad (S.A.W) anasema, “Wanadamu wote hukosea na kutenda hambi, lakini mbora wenu ni yule anayejirudi na kuomba toba.[2]Mwanadamu anayekosea na kutenda dhambi na kisha akajirudi na kuomba toba, huwa sawa na mwanadamu ambaye hajakosea wala kutenda dhambi.[3] Kufuatia ufafanuzi huu, tunaweza kusema kwamba mwanadamu anayekosea na kutenda dhambi kisha akajutia na kuomba toba kwa Mwenyezi Mungu, basi husamehewa na kujitakasa kama alivyozaliwa.

Katika hadithi nyingine Mtume Muhammad (S.A.W) pia anasema, “Endapo hamjatenda dhambi, basi Mwenyezi Mungu huwabariki na kuwajumuisha kuwa miongoni mwa wanaoomba toba. Njia ya pekee ya kujitakasa kutokanana dhambi au vitendo vibaya vinavyokiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu ni toba.  Mwenyezi Mungu pia anatwambia katika aya ndani ya Quran, “…Enyi mnao amini! Ombeni toba kwa wingi na Mwenyezi Mungu atawaongoa.[5]

Mwanadamu anapaswa kujibadili nafsi yake na kuomba msamaha kwa moyo wote. Hivyo basi anapoomba toba ya kweli, basi husamehewa na kutakaswa nafsi yake. Toba ya aina hiyo pia huimarisha imani ya wanadamu na kuzalisha matumaini mapya ndani ya nafsi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.

story@moodyhamza