Uwoya Ataja Sifa Za Mwanamume Anayemtaka.


Msanii wa kike wa filamu za bongo ambaye pia aliwahi kuolewa na mcheza mpira kutoka Rwanda mlimbwende Irene uwoya, amesema mpenzi wake wa sasa ana ngeu nyingi mwilini za kuchanwa visu.

Irene amesema watu kama hao ndio anaowataka yeye kwani inaonyesha uanaume halisi, na sio mwanaume anakuwa laini kama mtoto wa kike.
“Sijasema napenda wanaume wenye sura mbaya nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume, mwanaume uwe na ngeu, mimi bwana wangu ana ngeu, kachanwa visu yani”, alisikika Irene Uwoya akimfungukia Big Chawa.
Irene uwoya kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake tangu kuwe na tetesi za kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Msami na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi kwa watu.

Source: Udaku.

 

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors