Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia inasadikika hakuna kitu ambacho kina nguvu sana kama mahusiano ya mapenzi, hata hivyo kutokana na nguvu hiyo ya mahusino, watu wengi husaani mwanaume ndio ambao wanaathiriwa kwa kiwango kiubwa na nguvu hiyo.
Watafiti wa masuala ya mahusiano wanazidi kusema ya kwamba, mwanaume kila baada ya dakika tano ni lazima awaze masuala ya kimapenzi, hii ni kutokana wanaume wengi hupenda zaidi jinsia ya kike kwa kuona kwa macho. Ndo maana ukichunguza kwa makini wanaume huwa wanakuwa wanazingatia zaidi katika kutazama jinsia hii ya kike mahali popote walipo.
Hivi hujawahi ona wanaume wamekaa mahali wanapiga stori ghafla akapite mwanamke mzuri mbele ya macho yao ghafla stori zile zikasimama kwa muda? Bila shaka umewahi kuona. Utawasikia wakisema kwa minong’ono aaah angalia kifaa hicho, wapo wengine utawasikia wakisema mcheki chura huyo. Hii ina maana ya kwamba macho ya mwanaume ndio chanzo kikubwa cha kuingia katika mahusiano kabla ya kumjua tabia aliyonayo mtu huyo.
Lakini ukweli ambao upo nyuma ya pazia ni kwamba wanaume wengi huingia katika matamanio ya kimahusiono kwa kuona kwa macho zaidi tofauti na mwanamke. Hata hivyo mahusiano ya kimapenzi aliyonayo mwanaume ni matokeo ya macho yako. Kwa maneno mengine tunaweza kusema matamanio ya hisia za mwanamke yapo katika kuona zaidi kuliko kitu chichote.
Lakini ukienda upande wa pili wa shilingi, mwanamke huwa yupo tofauti sana ukilinganisha na mwanaume katika suala zima la kuingia katika mahusiano. Hisia za mwanamke huwa zipo zaidi katika maneno na mguso katoka kwa mwanaume. Hisia za mwanamke huwa hazipo katika kuona kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mwanaume.
Mwanamke huamini sana katika maneno ambayo ataambiwa na mwanaume, kwa mfano mwanamke akiambiwa anapendwa zaidi ya kitu chochote katika dunia hii mwanamke huamini hivyo,hivyo maneno ya mwanaume yana nafasi kubwa katika kuziteka hisia za mwabamke.
Lakini pia kama hiyo haitoshi mwanamke hupata hisia zaidi pale anapoguswa na mwanaume, hivyo ndo maana kama utakutana na msichana kwa mara ya kwanza atakaa usimguse katika mwili wake, hii ina maana mguso wa mwanaume una nguvu sana katika kuamsha hisia mwili wa mwanamke.
Hivyo kama ndivyo hivyo basi hii ni uofauti mkubwa ulipo kati ya mwanaume na mwanamke katika kuamsha hisia za kimapenzi. Na kitu kikubwa ambacho huongoza hamasa na kudumu katika mahusiona ya kimapenzi ni “mawasiliano” , mawasiliano ndiyo chachu kubwa katika mahusiano yenu. Hivyo kila wakati ili muweze kudumu katika mahusiano yenu hakikiasha unakuwa na mawasilino bora kati yako na mwenzi wako.
Source: Udaku