March 21 2017 kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kilifanya mazoezi yake uwanja wa Taifa Dar es Salaam chini ya kocha wao mpya Salum Mayanga, Taifa Stars inajiandaa na michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki iliyo katika kalenda ya FIFA.
Taifa Stars katika mwezi huu March itacheza michezo miwili ya kirafiki iliyo katika kalenda ya FIFA kati ya Burundi na Botswana itakayochezwa March 25 na 28 uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Kupitia afisa habari wa TFF Alfred Lucas amewatangaza manahodha wasaidizi wapya wa Taifa Stars.
Source: Millard ayo