Msanii wa Bongo Flava, Shetta amesema haamini kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja ni sababu ya kufanya vizuri.
Shetta ambaye amekaa kipindi kirefu bila kutoa ngoma, ameiambia EA Radio kuwa yeye anaamini katika kujipanga zaidi na kutoa ngoma kali.
“Mimi siamini kwenye kutoa nyimbo nyingi ndio ku-trend, nafikiri kujipanga kwangu ndio huwa kuna sababisha kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo, ningekuwa naweza kujipanga haraka ningeweza kutoa madude haraka lakini so far so good ngoja tutaibadilisha, ngoja tuone system yetu tufaifanyaje,” amesema Shetta.
Ameongeza kuwa, “naamini ukitoa kazi ambayo umejipanga nayo watu wanaweza wakaenyoy mwaka mzima au miaka miwili, kukaa kimya haijawahi kunihadhiri kwa chochote sana sana watu wananimisi lakini ninapokuja watu wanakuwa wananipokea, so am happy katika kitu ninachokifanya,” amesisitiza.
Source: Udaku