Izzo Business Aweka Wazi.

Rapa na staa wa ngoma ya ‘Rafiki’ aliyomshirikisha mrembo ‘Abela Music’ Izzo Business, amewaweka mashabiki katika hali ya utayari kuwa anafanyia kazi ujio wa album baada ya kipindi cha undani na uwepo wake katika muziki kwa takribani miaka 12 sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Izzo amebainisha kuwa ni muda sasa tangu yuko katika hatua za kuachia ngoma kali na kuutaja mwaka huu wa 2017 kuwa mwaka wa yeye kuachia album ambayo haikufahamika rasmi lini pia itakwenda kwa jina gani ingawa yapo maneno baadhi ambayo yametumika na kudhaniwa kuwa yanaweza kuwa kiasharia cha jina la album.

Hata hivyo Izzo akishirikiana na Abela music kwa sasa wanaendelea kufanya vizuri kupitia brandy yao ya biashara ya nguo ya ‘The Amaizing’ ambayo inaingia katika orodha ya Brandy Tanzania zinazotajwa kufanya vizuri sokoni mpaka sasa.

Source: Dizzim Online.