Sahihi ya Uislamu, maiti ana haki nne anazopaswa kutendewa, ambazo ni:

Ndugu msomaji, fahamu kuwa kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya Uislamu, maiti ana haki nne anazopaswa kutendewa, ambazo ni:

1. Kuoshwa,

2. Kuvishwa sanda,

3. Kuswaliwa, na

4. Kuzikwa.

Hii ina maana kuwa Waislamu watawajibika kuyafanya haya kwa kila maiti Muislamu na si vinginevyo. Na watakapoacha kumfanyia maiti mambo hayo watapata dhambi Waislamu wote wa sehemu ile.

Ndugu msomaji, tunafahamu kuwa una hamu kubwa ya kuyajua kiundani mambo manne tuliyoyataja hapo juu. Shaka ondoa, makala hii iliyo mikononi mwako itakuonesha hayo kadiri utakapozidi kufungua kurasa zake.

Awali ya yote tunapenda kukujulisha itikadi ya Uislamu kuhusu maisha na uhai huu wa dunia.

Ndugu msomaji, Waislamu wanaitakidi kuwa, kila kilichopo katika dunia kitaondoka (kitakufa). Na hii ni kutokana na kauli ya Allaah Aliposema:

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ

“Kila aliyekuwa juu yake (ardhi) ni mwenye kutoweka…” (Qur-aan 55: 26)

Kama ilivyozoeleka kuwa hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho, wala hakuna mchana usiokuwa na usiku, kadhalika hakuna uhai usiokuwa na mauti. Allaah Anasema:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ

“Kila nafsi itaonja mauti!…” (Qur-aan 21: 35)

story@moodyhamza