Mzee Chillo akiri pengo la Steven Kanumba.

Msanii mkongwe wa sanaa ya maigizo kutoka Tanzania Ahmed Olotu anayefahamika zaidi kwa jina la Mzee Chillo amekanusha maoni ya wengi ya kuwa tasnia ya filamu na maigizo Tanzania imekufa kwa kuwakosa baadhi ya waigizaji na waongozaji akiwemo muigizaji aliyepanda kwa kasi marehemu Steven Kanumba.

Amekiri kuwepo kwa pengo la Steven Kanumba na kuikataa sababu hiyo ya kutokuwepo kwake kuwa tasnia imeshindwa kuendelea na kuonekana kuwa inadidimia huku akifunguka zaidi na kuzitaja changamoto tofauti zinazoikumba tasnia ya filamu Tanzania kwa sasa.

Sources: Dizzim Online.