Rapa kutoka Tanzania anayefanya vizuri na ngoma yake ‘Mpe Habari’ aliyomshirikisha Rich Mavoko ‘Stereo’ amejibu kila swali linalomhusu kuanzia hatua za kufanyika kwa Remix ya Mpe Habari ambayo inawashirikisha wakali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania, kuhusu maisha ya kazi kama muajiriwa katika ofisi na kufanya muziki kama rapa ambapo pia katika kisikiliza uandishi wa Stereo imegundulika kuwa katika mistari ya Remix amemzungumzia rapa wa kike ambaye alishamchanganya kiamahaba ‘Chemical.
Stereo alimtaja Khaligraph kutoka nchini Kenya kuwepo kati ya wasanii waliochaguliwa kushiriki katika Remix ya kolabo hiyo ambapo mbele ya kameraa za Dizzim Online ameonekana Bill Nass na Stamina wakirekodi vipande vyao katika studio za Wasafi Record chini ya mtayarishaji wa siku zote kutoka katika studio hizo Lizer Classic.
Source: Dizzim Online