Nay Wa Mitego Auingilia Ugomvi.

Ni vuguvugu la masaa yasiyopungua 72 mitandaoni kwa wasanii wa Bongo Fleva ‘Diamond Platnumz’, AliKiba kisha akaongezeka Ommy Dimpoz huku kaionekana kwa mbali Abdul Kiba katika maneno na vijembe vyenye sura ya matusi vilivyoibuka mara tu baada ya kuachiwa, kusikika na kusambaa kwa kilichozungumziwa kupitia mistari aliyochana Diamond Platnumz katika Fresh Remix ya Fid Q ambayo pia imemshirikisha Ray Vanny.

Bila kwenda Nje ya mdundo wa ngoma ya ‘Fresh’ upepo uliendelea kuvuma isieleweke hatia yake ambapo baadae Diamond alipost kipande kifupi cha video ambayo anasikika akirap mistari ambayo liliongezea kasi ya mada zaidi mitandaoni.

Majibu ya kilichozungumziwa yalionekana kama yanaibuka kutokana na baadhi ya mashabiki kutafsiri kuwa kilichozungumzwa na Diamond Platnumz ni mishale ya Diss huku Tweets za AliKiba zilizoanza kumilimiminika kusemekana kuwa zinajibu mashambulizi. Picha la songombingo hilo likaendelea mapema jana ambapo Ommy Dimpoz alituma ujumbe uliokuwa sambamba na Picha yake aliyopiga akiwa na mama mzazi wa Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuweka maneno ya utata ambayo wengi hawakusifia kutokana na maudhui na tafsriri ya wazi wazi ya maneno hayo.

Rapa Nay wa Mitego akatumia muda wake kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kuandika maneno ambayo yalionekana kutoa onyo ya kuwa jambo la kutoelewana na kurushiana maneno kwa wasanii hasa wasanii husika yeye kwa upande wake alionekana kutolipinga bali alitoa angalizo kitu ambacho kitaeleweka kama maoni yake.

Hata hivyo hali hii imechukua sura pana hasa kwa mashabiki kulitolea maoni tofauti tofauti jambo hili huku kila mmoja akichangia wazo lake kutokana na jinsi alivyoelewa na kulipokea kama shabiki wa wasanii hawa wanaohusika.

Source: Dizzim Online.