Producer mkongwe wa Bongo Fleva, P-Funk amefunguka kwa kusema kuwa jina la kundi lake jipya ‘Bongolos’ limetolewa na mwanamuziki wa Marekani MIMS.
P-Funk amesema kuwa wazo hilo lilipatikana kupitia wimbo wa ‘You Can Never Be Me’ alioutayarisha yeye ambapo Jay Mo alisikika sambamba na MIMS miaka mitano iliyopita.
P-Funk amesema kuwa “Tangu tulivyopiga ile ngoma na tukapata vocal za MIMS na Jay Mo akaweka vocal na jamaa mwingine wa Marekani anaitwa Immu Cabir, kwenye verse ya MIMS alichana akasema ‘Welcome to the Jungle, Bongolos.
Alifafanua kuwa maana ya jina hilo ni Uafrika na utafutaji wa watu ambao ni kama wanaishi msituni.
Bongolos inayoundwa na wasanii wawili wameachia wimbo wao wa kwanza waliouita jina la ‘Wape’.
Kundi hilo lipo chini ya P-Funk Majani ambapo amedhamiria kuleta mapinduzi ya muziki wa Bongo Fleva kwasasa.
Source: Ishi kistaa