Mwanaume Mashine imeleta Mgogoro.

 


Mwanamuziki ambaye pia ni hit maker wa ngoma inayosumbua kwa sasa ijulikanayo kama “Mwanaume Mashine” Msaga Sumu amedai kuwa ngoma hiyo licha ya kumletea mafanikio ya muda mfupi kulinganisha na ngoma zote zilizopita lakini ngoma hiyo imeleta mtafaruku mkubwa katika ndoa yake kwa madai kuwa amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa madada wengi hapa mjini wengi wamekuwa wakimtaka kimapenzi mara baada ya kugundulika kuwa ana muhogo wa jang’ombe .

 

‘Wanawake wengi wamekuwa wakiahidi mambo kedekede ili mradi tu niwatimizie haja yao ya kimapenzi’ alisikika akisema hivyo msaga sumu ambaye pia aliwahi kutamba na ngoma ya UNANITEGA SHEMEJI.

Source: Udaku