Kifo cha mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mume wa Zari The Boss lady, Ivan Semwanga ni moja kati ya habari zinazozungumzwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kugusa hisia za wengi.
Baada ya Zari kuthibtisha kifo cha aliyekuwa mume wake, watu mbalimbali wamekuwa wakituma salamu zao za pole kwa familia wakionesha kusikitika kwa kuguswa na msiba huu ambapo miongoni mwa watu hao ni Miss TZ 2006 Wema Sepetu.
Wema aliandika kwenye account yake ya Instagram “Broken hearted…💔💔💔… Rest In Peace Ivan… 🙏🏼🙏🏼🙏🏼 … SHOCKING NEWS kwakweli… rambirambi zangu kwa familia nzima… Mungu awatie nguvu wale watoto jamani… 😔 bado ni wadogo mno… na Mungu amtie nguvu Mama watoto wako… utakua wakati mgumu kwenu lakini itapita”
Source: Millard ayo