Maneno ya Emmanuel Mbasha kuhusu kutumia gari ya watu

Kupitia U-HEARD ya XXL ya Clouds FM Mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha anadaiwa kuingia kwenye gari ya watu na kupiga picha kisha kupost kwenye mitandao ya kijamii bila ridhaa ya mwenye gari.

Mtangazaji Soudy Brown alipiga story na Mbasha ili kujua ukweli na akajibiwa hivi “Sifahamu na sijui kitu kama hicho, gari gani? mbona magari ninayopost yanafahamika ni ya kwangu, yanajulikana ninayomiliki mimi, sina gari jekundu nililowahi kupost… analalamika kwa lipi au anatafuta kiki? sifahamu kitu kama hicho.” – Emmanuel Mbasha

Source:  Millard ayo