BAD NEWS: Staa wa Kuch kuch hota hai amefariki leo…

Kuch kuch hota hai ni moja ya movie kali kutoka Bollywood ambayo imekuwa ikipendwa sana na wafuatiliaji wa filamu za kihindi hasa kutokana na uwepo wa Waigizaji mastaa kama Shah Rukh Khan, Salman Khan, Kajol na wengine.

Bad news iliyonifikia leo May 18, 2017 ni taarifa za kifo cha mmoja wa Waigizaji wa filamu hiyo Reema Lagoo ambaye amefariki mapema leo May 18, 2017 akiwa na umri wa miaka 59 ambapo katika filamu ya Kuch kuchi hota hai Reema Lagoo aliigiza kama mama wa Kajol akitumia jina la Mrs. Sharma.

Miongoni mwa filamu zilizompatia umaarufu ni pamoja na Kal Ho Naa Ho, Maine Pyar Kiya, Hum Aapke Hain Koun…!, Hum Saath Saath Hain, Jis Desh Mein Gangaa Rehta Hai na Vaastav.

Source: Millard ayo