Maneno ya Afande Sele kwa umarioo.


Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Afande Sele amedai kuwa vijana wa kiume kujihusisha katika mapenzi na wakubwa zao ili kusaidiwa kiuchumi ni moja wa sabubu zinazopelekea upungufu wa nguvu za kiume.

Afande Sele ameeleza kuwa kitendo hicho kinamnyima uhuru binafsi muhusika kwa sababu unapokaa na mtu ambaye kila kitu unamtengemea unakosa uhuru wa maisha.

“Hata uwezo wako wa kufikiri unapungua kwa sababu unajikuta muda mwingi unafikiria kumfurahisha mtu. Muda mwingine hata mapenzi unakuta hujisikii kwa sababu mapenzi nayo ni ratiba lakini kwa sababu unaishi na mtu anakulea utafanya tu.

“Ndio maana leo hii suala la nguvu za kiume limekuwa ni agenda kubwa kwa sababu wanafanya vitu na watu siyo machaguo yao ila wakijiari kwenye vitu kama kilimo watakuwa na maisha ya uhuru sana,” amesisitiza.

Source: Udaku

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!