Tyrese atoka salama.

Mwanamuziki, Muigizaji na Staa wa ‘Fast and Furious’ Tyrese Gibson ametoa taarifa za kuwa anaendelea vyema kiafya kupitia ujumbe ulioambatana na picha(Instagram) akionekana akiwa kashiliwa na mwane wa kike Shayla huku akiwa katika hali kujilaza kitandani na vifaa vya kimatibabu hospitalini.

 

Haikufahamika ni kipi kinachoisumbua afya yake kiasi cha kufanyiwa upasuaji lakini Tyrese aliishukuru zaidi familia yake kwa kuwa pamoja naye huku asiwasahau mashabiki kwa kumuombea katika wakati wote na muda wa takribani masaa matatu ya kufanyiwa upasuaji.

Tyrese kwa kipindi kirefu mpaka sasa anaoneana zaidi katika tasnia ya filamu na maigizo tofauti na miaka ya nyuma ambayo amekuwa akiwekeza muda wake mwingi katika muziki.

Source: Dzzim Online.

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors