Linah Asema Haya

 

 

Msanii Linah Sanga ‘Ndege Mnana’ amekanusha taarifa zinazoenea mtandaoni kuhusu suala la kujifungua na kuwataka watu wazipuuzie huku akiwasihi mashabiki zake waendeee kusubiri taarifa iliyo sahihi kutoka kwake na kwenye mitandao yake ya kijamii.

Linah amekanusha taarifa hizo kupitia EATV na kusema kwamba anashangazwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni huku akiwa hajui mtu anayesambaza taarifa hizo ana malengo gani.

“Hongera ya nini mbona mimi bado mjamzito? Sijajifungua bado na hata mwenyewe nashangazwa na huyo mtu aliyeanza kusambaza taarifa hizo ana malengo gani? Nawaomba mashabiki zangu waniombee kwa sasa hivi nikiwa nakaribia kwenda kujifungua hivi karibuni ingawa siwezi kusema ni lini kwani siyo vizuri, watu wanatakiwa waone. Mungu akinisaidia taarifa watazipata kupitia kwangu mwenyewe au kwenye mitandao yangu ya kijamii,” Linah alifunguka .

Katika hatua nyingine Linna ameongeza kwamba sababu ya za kutoonekana sana kipindi cha hivi karibuni hakujasababishwa na kisirani, hivyo kutoonekana kwake zipo sababu ya msingi.

“Ukweli nina sababu zangu za msingi zinazonifanya nisionekane, Ninachomshukuru Mungu kuwa na mimba hakujanifanya niwe kisirani ila baada ya ya sababu zangu kuisha nitaonekana kama kawaida. Niombeeni nijifungue salama”, aliongeza

EATV inamuombea mwanamuziki Linah maandalizi mema ya kumpokea mtoto wake wa kwanza.

Source: Udaku