Mara nyingi uwezo wa wototo kitaaluma hususani madarasa ya awali huelezwa na walimu au wazazi kutokana na matokeo ya mitihani, majaribio na mazoezi mbalimbali wanayofanya watoto hao wakilinganishwa na watoto wengine wanaosoma pamoja kwenye darasa moja.
Hata hivyo wataalamu Uingereza kupitia taasisi ya utafiti ya GL Assessment wameonya kuwa kumzungumzia mtoto au mwanafunzi kuwa ana uwezo wa kati yaani ‘average’ huwa ni sababu ya kuwafanya wanafunzi hao wasisogee mbele nakufanya vizuri zaidi kwenye masomo yao kwani kauli hiyo inawaaminisha kuwa huo ndio uwezo wao na hawawezi kupanda zaidi.
Kwa mujibu wa Mwanasaikolojia wa Elimu Poppy Ionides watoto wote wenye uwezo wa kati wanaweza kusaidiwa kufanya vizuri zaidi ya ilivyotegemewa lakini hii inahitaji shule husika kujenga mazoea ya kuwajengea watoto uelewa wa kuwa wanaweza kufanya vizuri zaidi ya wanavyofikiri.
Source: Millard ayo.