Diamond Platnumz Katuletea Majibu.

And the awards for the man of the year goes to  Diamond Platnumz. Well, man of the year kwa sababu za Kiafrika zaidi.. Utembezaji rungu ulioenda shule.. walau kwa tetesi zinazoendelea kuvuma. Si jambo geni kwa Chibudenga kuteka headlines kwa skendo za uvunjaji amri ya sita, lakini mwaka huu bombshells anazoangusha ni heavy weight – balaa kabisa kama za Hiroshima.

Na wakati mnadhani kubwa limetokea, linaibuka jingine kubwa zaidi ya lililopita. Skendo ya mtoto wa Hamisa Mobetto, Abdul Naseeb bado ipo pending… I mean jipu linasubiriwa litumbuke, kila mtu azinyake mbivu na mbichi, kwamba kweli Abdul ni damu ya Mondi? Wakati kila mtu anasubiria 40 ya Abdul ili macho yaione sura yake, lingine limeibuka wiki hii.

Mshindi wa Big Brother Africa, Dillish Mathews kaibuka kwenye picha na anataka awe starling kabisa, Hamisa kapigwa kikumbo. Ilianza kama mzaha katika ukurasa wa ‘the most influential Instagrammer of East Africa’ Mange Kimambi aliyejitahidi ‘kuconnect dots’ kwa picha kuhusu penzi jipya la Diamond na mrembo huyo wa Namibia na kwa kiasi fulani alimake sense, lakini haikutosha kuthibitisha.

Baadhi ya mashuhuda wa Zanzibar wakasema kuwa ni kweli walimuona Baba Tiffah katika hoteli ya kitalii ya Lagema visiwani humo akipunga upepo mwanana wa bahari Hindi, harufu ya karafuu na harua kwa mbali. Ni hoteli hiyo Dillish alifikia pia. Wengine wanasema wawili hao wana project, lakini project ndio iliyoanzisha uhusiano wa Zari na Diamond..

Watu wakaslide DM kwa Zari kumsanua kuwa ‘ebanaee, jamaa yako kama anakula mtoto mkali wa Kinamibia pande za Zenji, niaje niaje.’

“Oh you dming me to tell me how he cheated? So many dicks just like so many pussy on the market. Like why do people think ts all about fighting for dick? Honey I will fight for money not dick,” aliandika Zari kwenye Snapchat akimaanisha kuwa kuna wanaume wengi tu sokoni kama walivyo wanawake wengi. Pia anadai kuwa hana muda wa kugombania mwanaume kwakuwa ni pesa tu ndio ipo akilini mwake.

Kiufupi Zari amemind na uhusiano wake na Diamond upo matatani. Hii ni kwasababu amemnyooshea dole la kati mpiga picha wa Diamond, Kifesi aliyepost picha ya Mondi akioga maji ya bahari.

Hali hii inamweka Diamond kwenye kitimoto. Kwanini amekuwa mtu wa kumuumiza sana Zari? You can tell kwa picha zake, Mama Tiffah hana furaha siku za hivi karibuni. Anaweza kuwa anajipa moyo kuwa hajali, lakini ni mwanamke wa aina gani anayevumilia skendo za mpenzi wake zisizoisha? Ipo siku atachoka na pengine atafika ‘point of no return’ aseme hapana na couple hii inayopendwa sana Afrika Mashariki ifikie tamati.

Ikiwa hivyo, mashabiki watasikitika sana sababu uhusiano wao sio wao peke yao, wana kundi kubwa la watu linalowafuata nyuma na halipendi kinachoendelea. Labda ni muda wa Diamond kuuweka ujana pembeni na kukubali kukaa na mwanamke mmoja. For the sake of their children. This is too much.

Source: Dizzim Online.

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors