Jay Moe ataja nyimbo za wasanii alizowahi kuandika na anayetamani kumwandikia

Legendary wa Bongo Fleva Jay Moe ambaye ameachia wimbo mpya hivi karibuni unaoitwa ‘Nisaidie kushare’ ametangaza kuwa yupo tayari kumuandikia wimbo msanii yeyote akianzia na Bill Nass huku akizitaja baadhi ya nyimbo alizowahi kuandika kuwa pamoja na Aseme wa Q Chilah.

 “Natamani kumuandikia ngoma Bill Nass na mtu mwingine anayeimba. Niliwahi kuandika ‘Nilikataa’ pamoja na wimbo wa ‘Aseme’ wa Q chilla.” – Jay Moe.

Baada ya kusema hayo mkali wa hit song ‘Mazoea’ Bill Nass naye aliamua kuchangamkia fursa hiyo na kuandika haya kwenye Twitter ..>>>”Kwa Kuchangamkia Fursa !!Jay Mo Kaka Yangu Nakutumia Beat Mbili jioni ya leo Tukamilishe Story Ni Baraka Kwangu #NisaidieKushare”:-Bill Nass.

 

                            Source:Millard ayo