Jarida la Forbes limetoa list ya wafanya biashara 25 ambao ndio matajili zaidi barani Afrika mfanyabiashara kutoka
Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi kwa mujibu wa orodha hiyo ya mabilionea ya mwaka 2017.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo. Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.
Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni. Mo Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.
Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:
1. Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni
3. Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni
4. Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni
5. Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni
7. Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni
8. Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni
9. Isabel dos Santos, Angola
Utajiri: $3.1 bilioni
10. Issad Rebrab, Algeria
Utajiri: $3 bilioni
11. Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni
12. Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni
13. Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni
14. Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni
15. Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni
17. Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni
18. Folorunsho Alakija, Nigeria
Utajiri: $1.61 bilioni
19. Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni
20. Mohammed Dewji, Tanzania
Utajiri: $1.4 bilioni
21. Stephen Saad, Afrika Kusini
Utajiri: $1.21 bilioni
22. Youssef Mansour, Misri
Utajiri: $1.15 bilioni
23. Onsi Sawiris, Misri
Utajiri: $1.14 bilioni
24. Anas Sefrioui, Misri
Utajiri: $1.06 bilioni
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini
Utajiri: $1 bilioni
Source: Millard ayo